Skip to content

Kusoma

studyindenmark.dk  ni tovuti rasmi ya shirika la kimaitaifa la Elimu ya Juu nchini Denmark.

Taarifa zote kuhusu ufadhili, mitaala, maisha ya kusoma nchini Denmark  n.k. hupatikana  kwenye tovuti studyindenmark.dk . Unaweza pia kutembelea tovuti  ya Umoja wa Ulaya  kwa utafiti zaidi.

 Ni vema  ukafahamu kuwa Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania hautoi  ufadhili  ama habari maalum kuhusu Vyuo Vikuu vya Denmark. Taarifa zote zinapatikana katika Link iliyotolewa hapo juu.

Ili uweze kusoma  nchini Denmark ni lazima  uwe na kibali cha kuishi Denmark kabla ya kuwasili ambacho kinapatikana, wakati utakapo toa taarifa zifuatazo;

  • Uwejiunga katika elimu  ya Chuo Kikuu nchini Denmark;
  • Uwe na uwezo wa kujitegemea wakati unaishi nchini humo au uwe  umeshalipa  ada ya Chuo;
  • Uwe na uwezo wa kuongea nakuelewa lugha ya Ki-danish, Ki-swedish, Ki-norwgian, Kingereza au Kijerumani katika  kiwango cha kuridhisha.