Skip to content

Greenland

Greenland ilianzisha madaraka ya ndani tarehe 21 Juni 2009.

Greenland ina eneo la kiasi cha kilomita za milioni 2.2 na kukifanya kisiwa hicho kuwa kikubwa kuliko vyote duniani.

Theluji ndani ya kisiwa hicho inafunika takriban eneo la kilomita za mraba milioni 1.8 na kukifanya kisiwa hicho kuwa cha pili duniani kwa wingi wa theluji. Kuna baadhi ya sehemu ambayo theluji  inafikia ukubwa wa kilomita 3.5. Eneo la Kaskazini la kisiwa hicho, Cape Morris Jesup, ndiyo sehemu ya ardhi ambayo iko kiasi cha kilomita 730 kutoka North Pole.  Eneo la Kusini, Cape Farewell, liko katika eneo sawa na jiji la Oslo nchini Norway na Helsinki nchini Finland.