Skip to content

Utawala Bora

Denmark inasaidia Tanzania kikamilifu katika kuendeleza na kuimarisha haki za binadamu, utawala bora na demokrasia. Maeneo haya ni sehemu muhimu katika kuimarisha fursa ya nchi na kuweza kufadhili malengo ya muda mrefu ya maendeleo ya jamii katika nchi.

Ni Kwa nini Denmark inasaidia masuala ya utawala bora?

Utawala bora ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha mazingira mazuri katika sekta binafsi na kuongeza ufanisi bora katika utoaji wa huduma. Ni muhimu kuwa na Sekta ya umma ambayo  ina uwezo wa kukidhi mahitaji ya msingi ya watu na kutoa mfumo muhimu wa kukuza uchumi, maendeleo na kuongeza uwazi zaidi.

Ni namna gani  Denmark  inasaidia kintengo cha utawala bora?

Kuboresha utawala bora Tanzania inahitaji:

Wananchi, Bunge na vyombo vya habari vizidi kutaka kuona taasisi za serikali na serikali yenyewe zinawajibika ipasavyo;

Kuimarisha mifumo ya kuboresha uwazi, utekelezaji wa sheria, kanuni za mifumo na utaratibu.

Mpango wa utawala bora kutoka Denmark (2011-2015) umetenga kiasi cha DKK milioni 250 kwa ajili ya kuboresha utawala bora na kusaidia ugavi na  mahitaji katika sehemu tatu:

Mahusiano ya Kidemokrasia na Uwajibikaji:

Una fadhili na kusaidia mashirika ya jamii na  Tanzania Media Fund. Lengo la sehemu hii ni kufanya watanzania wafahamu haki na wajibu wao na kujenga jamii yenye uwazi.

Sekta ya msaada wa Kisheria:

Inalenga kuongeza msaada wa kisheria kwa kufadhili kituo cha huduma za sheria. Pia wanasaidia programu ya marekebisho ya sheria; Tanzania Legal Sector Reform Programme (TLRP).

Mafanikio

Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Tanzania imeshuhudia ongezeko kubwa katika uhuru wa kisiasa na kuboresha mfumo wa kudhibiti umeanzishwa. Serikali inazidi kuhojiwa na Bunge, wapinzani wa kisiasa, vyombo vya habari na mashirika ya kiraia juu ya masuala ya utawala. Mashirika ya kiraia yameongezeka kwa idadi na uwezo, na Bunge imeanzisha mchakato wa kisasa. Hata hivyo, changamoto kubwa bado zinaendelea.

Ingawa majukumu na wajibu wa Serikali na Bunge yanagawanyika ipasavyo, udhibiti na usimamizi kitaasisi bado havitoshi.  Hali hii inasababisha matumizi mabaya ya madaraka kwa serikali.

Japo uwezo wa mashirika ya kiraia, vyombo vya habari na bunge umeongezeka, taasisi hizi bado ni dhaifu. Pia, licha ya mafanikio makubwa katika uchaguzi mkuu wa 2010, bado wapinzani wa kisiasa ni dhaifu na wamegawanyika. Zanzibar, utawala bora na heshima kwa uhuru wa kisiasa  umebaki mdogo.