Skip to content

Ubia wa Biashara Danida

Mpango wa ubia wa biashara (DBP) ambao uko kwenye sekta ya Danida kwa muda mrefu inasaidia ushirikiano wa faida za kibiashara kati ya makapuni ya Denmark na Tanzania. Kuanzia mwezi wa nane mwaka 2011 mpango wa zamani wa Biashara kwa Biashara; Business-to-Business (B2B) na Ubunifu wa maendeleo ya Ushirikiano; Innovative Paterneships for Development (IPD) umebadilishwa nafasi na mpango huu wa (DBP). 

Nani anaweza kujiunga?

Mpango huu wa DBP umetengenezwa kwa ajili ya kukuza uchumi na kupunguza umasikini.  Huu mpango unafanikishwa na msaada wa muda mrefu kati ya makapuni ya Tanzania na Denmark, ambayo yana lengo sawa la kibiashara.

Mapendekezo ya  mradi huu yatatolewa na makapuni ya Kitanzania yatakayoingia ubia na makapuni ya nje, au kampuni za Denmark zenye kutafuta fursa ya uwekezaji katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mbali na  Biashara endelevu, kila mradi utahakikiwa kutokana mchango wake katika maendeleo ya nchi kwa mfano upatikanaji wa nafasi za ajira, ustawi wa jamii, utuzaji wa mazingira, utengenezaji wa bidhaa za kuuza nje, usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake, uboreshaji wa mazingira, na mipango ya CSR.

Programu hii inalenga miradi yenye kuleta matokeo makubwa. Miradi itakayopewa kipaumbele  ina sura ya utengamano katika Jumuiya ya  Afrika Mashariki

Ni nini unachoweza kuomba?

  •  Programu hii  inatoa msaada wa kuanzisha miradi ya ubia:
  •  Utapatikanaji wa ubia
  •  Mafunzo ya biashara
  •  Uchambuzi wa awali
  •  Msaada wa kitaalamu
  •  Kukuza biashara ya nje
  •  Kuboresha mazingira ya ndani na nje
  • Kuboresha mazingira na mpango wa CSR