Skip to content

Sera Mpya ya Nchi

Je unataka kujua jinsi ushirikiano wa Denmark na Tanzania utakuwa na sura gani miaka minne ijayo? Basi soma sera mpya ya nchi, iliyoandaliwa na serikali ya Denmark. Unaweza kusoma juu ya sera hii kulia ya ukurasa huu.

""

Sera hii inaelezea jinsi Serikali ya Denmark inavyoona changamoto na fursa zilizoko nchini Tanzania, pamoja na lengo la mkakati ambao ni endelevu katika ushirikiano huu kuanzia mwaka 2014 hadi 2018. Mkakati huu umetengenezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

Ni nini Dira ya Sera hii?

Dira ya ushirikiano huu ni kuhakikisha kwamba Watanzania wote wawe wanawezeshwa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi na kuhakikisha wanaendeleza historia yake ya amani, demokrasia, na maendeleo. Kwa ujumla lengo hili linaelezea jinsi gani mkakati wa ushirikiano kati ya Denmark na Tanzania utasadia serikali ya Tanzania kwenye maeneo yafuatayo:

1.  Kupunguza umasikini, kutofautiana  na kuhakikisha upatikanaji sawa wa huduma za kijamii;

2.  Kukuza  na kuboresha hali ya mazingira, ajira na;

3. Kuimarisha demokrasia, utawala bora, utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu.

Ni vitu gani vinapaswa kuungwa mkono?

Ili kufikia malengo ya mkakati huu, katika maeneo yafuatayo:

1.  Sekta ya Afya

2.  Sekta ya Kilimo

3.  Umuhimu wa kuhakikisha utawala bora na haki za dinadamu kwa wote

4.  Amani na utulivu wa Kikanda

Njia Mpya

Ushirikiano wa kimaendeleo utaendelea kuwa nguzo muhimu, katika ubia ambao pia utaimarishwa  katika maeneo mengine; hususan mahusiano ya kibiashara na ushirikiano wa kisiasa, kikanda na kimataifa.