Skip to content

Mkakati wa Pamoja

Mkakati wa pamoja wa msaada kwa Tanzania (JAST) ulizinduliwa mwaka 2007. Huu ni mpango kamilifu wa kusimamia ushirikiano wa kimaendeleo nchini Tanzania kati ya Serikali na Nchi walisaini na mashirika ya kimataifa. 

Mkakati huu unalenga zaidi  misaada  yenye tija na ushirikiano katika utekelezaji wa mkakati wa kupunguza umasiskini. Mkakati wa pamoja  wa msaada Tanzania utaboreshwa mwaka 2014 na nafasi hiyo itabadilishwa  na mpango mpya wa maendeleo  (DCP) ambao unakamilishwa na  Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo

Mkakati wa pamoja wa msaada kwa Tanzania (JAST) uliandaliwa kwa kuzingatia ahadi na mipango ya kitaifa na kimataifa kuhusu misaada yenye tiya hususan azimio la Paris kuhusu misaada yenye tiya kuanzia mwaka 2005. Lengo la Mkakati wa pamoja wa msaada kwa wa Tanzania ikifuatiwa na mpango mpya  wa ushirikiano ni kuchangia utekelezaji wenye ufanisi wa mpango wa taifa wa kukuza  uchumi na kupunguza  umasikini (MKUKUTA) na mpango wa kukuza  uchumi zanzibar (MKUZA). Kanuni mbili za msingi ni uhuishwaji kati ya wahisaini na kulinganisha  na mifumo ya Serikali.