Skip to content

Masuala ya Kijinsia

Denmark inaunga mkono Tanzania  kuendeleza usawa wa Kijinsia na uwezeshaji wa wanawake. Kuwaendeleza wanawake kwa kuwapa fursa sawa katika kushiriki na kufanya maamuzi na kuongeza uwezo wa kumiliki jambo muhimu katika kupata maendeleo endelevu kwa wanaume na wanawake.

""

Ni kwanini Denmark inaunga mkono usawa  wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake?

Usawa wa kijinsia unamaanisha kwamba wanawake na wanaume wanaweza kufurahia hali ya usawa na kuwa na nafasi ya kutamubua haki zao za kibinadamu; na uwezo wa kuchangia  maendeleo ya Taifa, kisiasa kiuchumi, kijamii na kiutamaduni, na kunufaika na matokeo yake. Usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake ni nyezo muhimu kwa maendeleo ya Taifa lolote Dunia. Awali iliaminika kuwa usawa wa kijinsia unaweza kufanikiwa kwa kuwapa wanawake na wanaume fursa sawa, hata hivyo uzoefu umeonyesha kwamba hivi sivyo. Hivi sasa dhana ya usawa wa kinjisia imedhihirisha kwamba wakati mwingine wanawake na wanaume wanahitaji utendaji tofauti ili wafikie matokeo sawa.  Hii  inatokana na hali tofauti za maisha au kufidia ubaguzi uliokuwepo awali. Ni wazi kwamba ukosefu wa uwezeshaji wa kiuchumi wa wanawake na unyanyasaji wa kijinsia (GBV) ni vikwazo viwili  vikubwa kwa wanawake kufurahia kikamilifu haki zao za kibinadamu. Zikiwa kama chachu ya mabadiliko, haki za binadamu zikizingatiwa zinasaidia kupambana na misingi inayoendeleza ubaguzi wa wanawake na wasichana nchini Tanzania. Kwa njia za uwezeshaji na upashanaji habari kuhusu haki za binadamu, wanaume na wanawake watahamasika na kudai uwajibikaji wa viongozi wao.

Ni kwa  jinsi gani Denmark inasaidia  usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake?

Mradi wa Denmark wa kusaidia mkakati wa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake  (2012 -2014) wenye kiwango cha fedha za Denmark  DKK 25 milioni una lengo la kuimarisha hali ya maisha ya wanawake nchini kwa kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake:

Sehemu 1 : Unyanyasaji wa Kijinsia: Kwa kusaidia Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania, (TAMWA) Sehemu hii imelenga kuboresha na kuzuia unyanyasaji wa kijinsia kwa kubadilisha na kuimarisha mfumo wa sheria na taratibu kwa ajili ya maslahi ya umma na jamii. Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania kwa kushirikiana na Mtandao wa Kijinsia wa Wanawake, Chama cha Wanawake, (TAWLA) Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZAFELA) na Shirika la Usuluhishi wa Migogoro (CRC) itawezesha kuwepo kwa ufanisi wa huduma zote zinazohitajika.

Sehemu 2: Uwezeshaji wa wanawake Kiuchumi: Sehemu hii inalenga kuwezesha wanawake kiuchumi kwa kuimarisha mfumo wa mtandao na ujuzi wa biashara, upatikanaji wa masoko na mikopo na ufahamu wa haki zao. Mpango huu unatekelezwa katika ngazi ya chini na kikundi cha wanawake kinachoitwa (WISE) wakishirikiana na vikundi vingine vya wanawake katika jamii. Kipengele cha pili katika sehemu hii, itahusu mpango utakaowawezesha wanawake kupata fedha Woman’s Access to Finance Intiative (WAFI) lengo likiwa ni kuwasaidia wanawake waliotayari kufanya biashara ndogo ndogo, na za kati. Wanawake hao watapata mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaaam, Shule ya Biashara (UDBS) na fursa yakupata mkopo kutoka benki ya CRDB  Tanzania.

Mafanikio

Tanzania imepiga hatua kubwa katika kufikia usawa wa kijinsia, kupitia utekelezaji wa sera husika kuanzia miaka ya 2000. Hatua hizo ni pamoja na uandaaji wa mazingira mazuri ya kijinsia kisera na sheria nchini. Utekelezaji huu umesababisha  kuridhiwa kwa mikataba muhimu ya kimataifa na kikanda kama CEDAW na Itifaki ya SADC kuhusu usawa wa kijinsia. Aidha hatua zilizotekelezwa kikanda na kimataifa ni pamoja na kuingizwa vifungu vya haki za wanawake  katika Katiba ya nchi na iliyopelekea kuongeza kwa  idadi ya wanawake katika Bunge na Mabaraza ya Serikali za Mitaa.  Kuimarishawa kwa sheria kama vile Sexual Offenses Special Provision Act (SOSPA) 1998 ambayo inalenga kulinda heshima na utu wa wanawake na watoto, kuwepo kwa sera ya kitaifa na seraa ya wanawake na jinsia (2000) na mkakati wa kitaifa kuhusu usawa wa kijinsia (2005).

Hata hivyo ingawa Tanzania ina sera nzuri za marekebisho ya sheria na mikakati ya kupunguza umasikini yenye viashiria thabiti vinavyozingatia jinsia bado hayajafanikiwa kuwa na matokeo endelevu ya usawa wa kijinsia hasa katika maisha ya wanawake na wasichana walio wengi. Changamoto Kuu udhaifu katika utekelezaji wa mkakati  iliopitishwa katika ngazi mbalimbali na vikwazo sugu ambvyo havijashughulikiwa kuziba pengo kubwa  kati ya utekelezaji wa sera juu ya usawa wa kijinsia na kuleta mabadiliko katika ngazi ya mitaa.

Sababu zinazopelekea hali hii ni pamoja na utashi mdogo wa kisiasa na uongozi juu ya usawa wa kijinsia katika baadhi ya ngazi ndani ya miundo ya Serikali  na uwajibikaji na uratibu usio na tija katika kukuza usawa wa kijinsia.  Matokeo yake ni udhaifu tuu katika umiliki na uwajibikajii wa ajenda hii muhimu ya haki za kijinsia.

Kuna vipingamizi kadhaa vinavyo sababisha mafanikio madogo katika mradi huu. Baadhi ya viongozi na watendaji wa siasa na Serikali hawajaupa kipaumbele mradi huu. Uwajibikaji ni mdogo kwenye kuratibu na kusimamia ukuwaji wake. Mapungufu haya  yanasababisha umilikaji na uwajibikaji wa mradi huu muhimu wa wanawake kubaki dhaifu. Pia kuna dhamira  potofu kuhusu usawa wa kijinsia miongoni mwa jamii. Haya yote yanachangia kusuasua kwa mradi huu. Pia kuna changamoto kubwa kutokana na mifumo dume iliopo kwenye sera ya maendeleo ya jamii.