Skip to content

Sekta ya Biashara

Danida imekuwa ikisaidia Tanzania katika sekta ya biashara tangu miaka ya 1990. Nia ya msaada huu ni kutengeneza mambo ambayo yana ruhusu  biashara ikuwe, iwe  na uendelevevu na kujingiza kwenye mashindano ya kibiashara. Mpango  huu kwa hivi sasa uko kwenye awamu ya nne, ambayo kiwango chake cha fedha ni DKK 600 milioni kwa kipindi cha 2013 hadi 2019.

Women shopping at grocery

Msaada huu unawasilishwa na Mpango wa Sekta ya Biashara  inaoitwa Business Sector Programme Support (BSPSIV). Lengo la awamu hii ni kusaidia wakulima wa kima cha chini na biashara ambazo zinazohusika na kilimo kama usindikaji mazao ya kilimo ambao unaongeza thamani kwenye mazao.

Nia ya awamu hii ya nne ni kuongeza ajira na mapato ya wakulima, usajiri ambao ni mikro, mdogo na wa kati;  Mirco, small and Medium enterprises (MSMEs). Fursa hii ya awamu ya nne itatekelezwa kwa njia ambayo inazingatia mazingira mazuri na kuakikisha kwamba biashara inatekelezwa kwenye hali ya heshima na haki za binadamu zinazingatiwa. Mpango huu una lengo la kuongeza mapato ya wakulima 300,000 na kujenga makazi 100,000. Waaidha wa mpango huu unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za fedha kwa Watanzania milioni 2.

Awali za awamu zilizopita: awamu ya kwanza na awamu ya pili, kilianzishwa mwaka 1998 hadi mwaka 2003. Awamu ya tatu (BSPSIII) yenye  kiwango cha fedha za DKK milioni 550, ilianzishwa mwezi wa saba mwaka 2008 na zitamalizika mwaka 2014.

Ni kwa nini Denmark insaidia sekta ya biashara?

Dhamira ya Denmark ni kuchangia katika dira ya Tanzania kuwa nchi ya mapato ya kati mwaka 2020. Uchambuzi umeonyesha kwamba Tanzania inahitaji biashara yenye mashindano ambayo itaweza kujenga mali nchini, makazi halisi,  na kuchangia katika mapato ya serikali kwa kulipia kodi.

Ni jinsi gani Denmark inasaidia sekta ya Biashara?

Mpango wa sasa wa sekta ya biashara umetengenezwa kuangalia sababu ambazo zina sababisha udhibiti wa ukuzaji na ujengaji wa makazi katika sekta binafsi. Mpango huu utatekelezwa katika ari 3 maalumu:

Maendeleo ya masoko ya Kilimo: eneo hili ni muhimu sana katika mpango wa sekta ya biashara. Nchi ya Denmark kwa kushirikiana na wawekezaji wengine nchini Tanzania, watasaidia wakulima na biashara ambazo zinajihusisha  na mazao ya mafuta ya alizeti na uzalishaji wa mahindi na kunde. Umuhimu wa msaada huu ni kuwawezesha wakulima na wafanya biashara kupata masoko ya bidhaa za. haya Mwenedo huu utasaidia kuondoa vikwazo ambavyo vinasababisha wakulima na wafanya biashara wasifikie malengo. Hatua hii itasaidia kuongeza thamani kwa bahadhi mazao ambayo yata fadhiliwa na kusimamiwa na Maendeleo ya Masoko ya Kilimo; Agricultural Markets Development Trust (AMDT). Kitengo hichi kitafadhiliwa kifedha na nchi za Denmark, Sweden, Ireland  na Switerzland.

Kuboresha mazingira ya Biashara: Serikali za mitaa na mamlaka na washirika wa biashara ya mioka ya Dodoma na Kigoma, imeteuliwa ainisha vikwazo vinavyokwamisha  ukuwaji wa biashara na kuboresha utekelezaji wa mfumo wa sheria uliopo. Uwekezaji wa kwenye miradi midogo, midogo utafadhiliwa ili kuwepo na uwezo wa kutambua vikwazo na kusadia kufungua uwezo wa biashara na kukuza maendeleo ya uchumi.

Kuboresha upatikanaji wa fedha: Lengo la mpango huu ni kuwekaza fedha kwenye ujasirimali midogo na wakati, fedha za kilimo na pesa zinazopatikana kwa njia ya mitandao ya simu za viganjani. Msaada huu ni msaada ambao ni endelevu na unasambazwa na kitengo cha Financial Sector Deepening Trust (FSDT) na Msaada wa Sekta Binafsi wa Kilimo; Private Agriculture Sector Support (PASS) Trust. Mashirika haya mawili yamefanikiwa katika kufadhili msaada wa fedha kwa watanzania walio wengi. Uendelevu wa msaada huu utawezesha PASS na FSDT na kuwafikia  walengwa wengi wa mradi wa watu  MSMEs, ambao ni wakulima, na wafanya biashara ya mazao ya kilimo.