Skip to content

Afya

Serikali ya Denmark kwa kupitia shirika lake la maendeleo linalojulikana kama Danida, imesadia kuboresha huduma za afya Tanzania kwa miongo kadhaa tangu mwaka 1996. Msaada huu umetolewa kwa kupitia mpango wa Danida wa Sekta ya Afya unaojulikana kama Health Sector Support Project ambao kwa sasa uko katika awamu ya nne (HSPS IV). Awamu hii ni ya miaka mitano na utekelezaji wake umeanza mwaka 2009 mpaka 2014. Kiasi cha fedha kilicho tengwa kutekeleza mpango huu ni DKK 910,000,000 ambazo ni sawa na dola za Kimarekani milioni 163.1. Danida inaendelea kuchangia uboreshaji wa Sekta ya Afya na Ukimwi kwa kupitia utaratibu wa msaada wa Bajeti Kuu ya Serikali, ambayo lengo lake ni kuendeleza ufanisi wa misaada inayotolewa.

Baby in arms - Embassy of Denmark

Ni kwa nini Denamrk inasadia Sekata ya Afya?

Madhumuni ya msaada wa Denmark katika sekta ya afya ni kuboresha hali ya afya na ustawi wa watanzania wote kwa ujumla. Mkazo maalum wa mpango huu, unazingatia kuhudumia makundi maalaumu kama wanawake, watoto na wasiojiweza. Msaada wa sekta ya afya unatoka katika ushirikiano wa fedha za Tanzania Bara, na mipango ya mkakati wa afya wa Zanzibar, pamoja  na Mkakati wa Pili wa kupambana na ugonjwa wa Ukimwi, The second National Multi-Secoral Strategic Framework on HIV/AIDS (2008 -2012). Mipango  yote hii iko ndani ya mpango wa pili wa Taifa wa kukuza  uchumi na kuondoa umasikini kwa  Tanzania Bara Mkukuta II na mpango wa pili wa kukuza Uchumi kwa Zanzibar  Mkuza II, pamoja na mikakati ya sekta ya Maendeleo ya Milenia. Malengo haya yanalenga pia uboreshaji wa afya ya uzazi na mtoto na kupambana na VVU/UKIMWI.

Ni jinsi gani Denmark inasaidia Sekta ya Afya?

Msaada wa Denmark katika sekta ya Afya umegawanywa katika sehemu tatu:

Sehemu ya kwanza: Tanzania Bara

Lengo la msaada huu ni kusaidia utekelezaji wa Sekta ya Afya katika Mkakati wa tatu wa utekelezaji  na Uboreshaji wa Huduma za Afya Health Sector Strategic Plan III, pamoja  na kuboresha utoaji wa huduma za Afya ya msingi kwa kiwango kinachokubalika, kwa gharama nafuu na endelevu. Huduma hii inawalenga wale walioko hatarini ili kuboresha afya zao na ustawi wao kwa ujumla.

Fedha nyingi za mradi huu zinatolewa kupitia kwenye mfuko wa ushirikiano wa pamoja wa wafadhili na serikali ya Tanzania kwa ajili  ya kuboresha hudma za Afya unaojulikana kama Health Basket Fund. Lengo la kuanzishwa kwa mfuko huu ni kusadia serikali kutekeleza Mkakati wa Tatu wa Utekelezaji na Uboreshaji wa huduma  za Afya Health Sector Strategic Paln III amabo unatekelezwa katika ngazi zote; kuanzia jamii, vituo vya afya na zahanati, ngazi ya wilaya mikoa na kitaifa.

Adhia, sehemu nyingine ya fedha za mpango huu zinatumika kuimarisha  mifumo ya afya kujenga uwezo katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kama vile msaada wa kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi kwenye huduma za Afya, Public-Private Paternship (PPP).

Serikali ya Denmark kwa kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imeajiri wataalamu watano kutoa ushauri  katika maeneo mbalimbali hususan yale yanayonufaika na msaada inayotolewa na Denmark.

Kiasi kilichotengwa kwa ajili ya kusaidia huduma za afya kwa upande wa Tanzania Bara ni DKK 528, 000,000 sawa na dola za kimarekani 93,000,000 kwa kipindi cha miaka mitano.

Sehemu ya pili ya mradi huu: Zanzibar

Lengo ya sehemu hii ya pili ni kusaidia utekelezaji wa Mkakati wa Pili wa kuboresha huduma za Afya Tanzania Visiwani Sector Strategic Plan II Zanzibar. Ili kuhakikisha usawa katika upatikanaji wa huduma bora za afya kuweka makzo kwenye nganzi ya wilaya. DANIDA imetoa washauri wawili na ofisa mmoja katika ofisi ya Wizara ya Afya Zanzibar ili kusaidia katika utekelezaji wa mpango huu huko visiwani.

Kisasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya Zanzibar ni DKK milioni 120 sawa na dola za Marekani milioni 21. Denamrk pia inchangia katika mfuko wa pamoja wa afya ujulikanao kama Health Basket District Sub-Vote Fund. Mfuko huu ni kwa ajili ya kutoa huduma za afya wilayani na kusaidia sekta  ya afya katika upatikanaji  wa madawa na vifaa vya matibabu pamoja na ununuzi na usambazaji, na usimamizi wa utoaji wa huduma za afya kwa ujumla.

Sehemu ya tatu ya mradi huu: insadia katika kupambana na vita dhidi ya VVU/UKIMWI

Sehemu ya tatu inalenga kusadia utekelezaji wa Mpango Shiriki wa Taifa katika kupambana na maambukizi ya Ukimwi, National Multi-Sectroal Strategic Framework (NMSF).

Fedha zilizotengwa kwa ajili ya sehemu hii ni Dkk milioni 220 ambazo ni sawa na dola za Kimarekani milioni 38.8.

Kwa upande wa Ukimwi kupitia NMSF, fedha zinazotolewa wilayani, ni kwa ajili ya huduma zisizo za kitabibu non-medical HIV/AIDS intervations. Fedha  hizi zinatolewa kupita katika Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) ili kusadia uimarishaji wa uwezo na ujenzi  wa ofisi mpya.

Fedha nyingine za Ukimwi zinatolewa kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali kupitia kwa Rapid Funding Envelope (RFE) na Femina HIP.

Mafanikio katika Sekta ya Afya

Mfuko wa Fedha  za pamoja Health Basket Fund umechangia katika kuwepo na mafanikio mbalimbali katika sekta ya afya. Mafanikio makubwa yamekuwepo katika kupunguza idadi ya vifo kwa watoto wachanga katika Tanzania Bara. Kati ya mwaka 2005 na 2010, idadi ya vifo vya watoto imepungua kwa kutoka  vifo 112 mpaka 81 kwa kila watoto 1,000 waliozaliwa hai, na kutoka vifo 68 mpaka 51 kwa watoto 1,000 kwa watoto chini ya miaka mitano. Matokeo haya ya mechangiwa na mambo kadhaa, kama vile utoaji wa chanjo na ugawanyaji wa Vitamini A.

Maambukizi ya VVU yamepungua kutoka asilimia 7% mwaka 2003/2004 – kufikia asilimia 5.1% katika mwaka 2011/2012.

Maendeleo mazuri yamepatikana katika kuzuia na kutibu malaria na ongezeko kubwa la idadi ya watoto chini ya miaka mitano ambao wanatumia chandarua yenye dawa. Mwaka 2005-2012 asilimia iliongezeka  kutoka 16% hadi 72%.

Vifo vya wajazito navyo vimepungua kutoka 578-454 kwa kila wanawake 100,000 wanaojifungua, kati ya mwaka 2005 na 2010. Mafanikio haya yalikuja baada ya miaka mingi ya maendeleo madogo sana, hata hivyo juhudi zinatakiwa ili kupunguza vifo vya kina mama ili kufikia malengo ya milenia.

Ni muhimu wakati huu kuzingatia usawa na utoaji wa huduma bora za afya kwa ushirikiano wa  Serikali ya Tanzania na mashirika ya maendeleo.