Skip to content

Jumuiya ya Afrika Mashariki

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ina idadi ya Watu zaidi ya milioni 141 na pato lake la taifa ni USD 99 bilioni. Lengo La msaada wa Danida ni kuongeza utangamano wa kikanda, ushindani, katika soko la kimataifa na kuvutia wakezaji wa kigeni.

Thorning-Schmidt na Sezibera

Picha: Helle Thorning-Schmidt na EAC Secretary General Richard Sezibera


Ni kwa nini Denmark inasaidia Jumuiya ya Afrika Mashariki?

Utangamano wa kikanda ni sehemu ya mkakati wa DANIDA  kwa ajili ya maendeleo. Utangamano wa nchi za Afrika Mashariki utaimarisha zaidi Jumiya hiyo katika soko la kimataifa na kuvutia wawekezaji wa kigeni. Hii itanufaisha raia wa nchi tano ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda hususan katika upatikanaji wa bidhaa zaidi, mishahara bora na uhuru wa kutembeleana.

Ni jinsi gani Denmark inasaidia Jumuiya ya Afrika Mashariki?

Denmark inatoa msaada wa kiasi cha DKK 160,000,000 (sawa na USD 28,700,000)  kwa ajili ya mtangamano wa kikanda katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Baadhi ya maeneo, yanayo jadiliwa na DANIDA kuhusu msaada huu ni:

Trademark East Africa: Shirika hili linasaidia Jumuiya ya Afrika Mashariki katika eneo la biashara na ushirikiano wa kikanda kwa lengo la kuboresha ufanisi katika sekta ya miundombinu na kujenga uwezo ndani ya Wizara, Idara na Mashirika yanoyohusika katika mchakato mzima wa utangamano. Aidha, Shirika hilo linaisadia Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mfuko wa ubia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki: Mfuko huo una lengo la kusaidia kukuza utekelezaji wa Umoja wa Forodha na Soko la pamoja.
Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki upande wa kushoto.