Skip to content

Bajeti Kuu ya Serikali

Denmark inachangia Bajeti Kuu ya Serikali; General Budget Support (GBS) tangu mwaka 2001. Lengo la msaada huu ni kukuza uchumi na kupunguza  umasikini.  Programu hii ya GBS ambayo iko kwenye awamu ya nne (2011-2015) imetenga fedha za msaada kiasi cha DKK 615 milioni ambazo  ni  sawa na dola milioni 110 za Kimarekani. Takriban asilimia 20 ya fedha hizi zinategemea mafanikio ya mwaka hadi mwaka katika sehemu zilizochaguliwa.  

Girls washing pans - by Mikkel Oestergaard

Ni kwa nini Denmark inachangia Bajeti Kuu ya Serikali?

Bajeti Kuu ya Serikali inachangia kukuza uchumi wa Tanzania na kupunguza umaskini kwenye maeneo yote. Hii inafanyika kwa njia ya kusaidia utekelezaji na ufuatiliaji wa Mkakati wa pili wa Kukuza Uchumi na kupunguza Umasikini, unaoitwa (MKUKUTA II) na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Tanzania (FYDP). Kwa kuchangia Bajeti Kuu ya Serikali, Denmark inakusudia yafuatayo:

 • Kukuza uchumi na kupunguza umasikini kwa kutoa fedha kwenye sekta ya jamii
 • Kuboresha umilikaji wa maendeleo ya Tanzania na kuhakikisha kuwa serekali inawajibika kwa raia wake na sio kwa wafadhili
 • Kuboresha matumizi ya serikali na usimamiaji wa fedha.
 • Kushirikisha  mazungumzo kuhusu sera ili kuboresha mikakati ya kukuza uchumi na kupunguza umasikini.
 • Kuimarisha uwezo wa watekelezaji wakuu wa mkakati wa kupunguza umasikini - Mamlaka za Serikali ya Mitaa.

Ni jinsi gani Denmark inachangia Bajeti Kuu ya Serikali?

Awamu ya nne ya Bajeti Kuu ya Serikali Tanzania ilianza katikati ya mwaka 2011 kwa kiwango cha DKK 615 milioni (ambazo ni sawa na dola 110 milioni za Kimarekani) kwa muda wa miaka 2011-2015. Takriban asilimia 20 ya fedha hizi zimewekwa kwenye Potential Annual Performance Tranches, kwa ajili ya kuhamasisha na kupongeza utendaji wa baadhi ya maeneo mbalimbali nchini kila mwaka.

Kwa sasa nchi 12 wahisani zinachangia Bajeti Kuu ya Serikali nchini Tanzania na kiwango cha fedha kilichotengwa mwaka 2013/14 ni dola za Kimarekani 560 milioni.

Matokeo na Changamoto

Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazoongoza katika kupewa misaada kwenye Bajeti Kuu ya Serikali na uiano wa misaada ya wafadhili. Bajeti Kuu ya Serikali pamoja na ongezeko la ukusanyaji wa kodi imeweka msukumo  katika ukusanyaji wa kodi na matumizi ya umma, Hii imepelekea kupanuka kwa utoaji wa huduma hususan katika eneo la Afya na Elimu.

Hata hivyo, utafiti unaashiria na changamoto zinazohusu juhudi za kupunguza asilimia ya kaya ambazo ni fukara kwa mantiki hiyo, Serikali ya Tanzania na Washirika wa maendeleo wanaafiki yafuatayo:

 • Kuunga mkono juhudi za kupunguza umaskini
 • Kuimarisha mazingira ya biashara
 • Kuboresha utoaji na ubora wa huduma za kijamii 
 • Kuimarisha usimamizi wa fedha za Umma
 • Kuendeleza ukuaji wa uchumi
 • Kuhakikisha mapambano yenye tija dhidi ya rushwa.

Awamu Mpya

Programu mpya ya Bajeti ya Serikali inaandaliwa na itaanzishwa rasmi mwanzo wa mwaka wa fedha 2014/2015.