Skip to content

Danida

Haki ya Maisha Bora ni mkakati wa Denmark wa maendeleo. Lengo la mkakati huu ni kupambana na umasikini, haki za binadamu na ukuzaji wa uchumi.

Mkakati wa Msaada wa Maendeleo kutoka Denmark

Mkakati wa Haki ya Maisha Bora, unajenga msingi madhubuti wa ushirikiano wa kimaendeleo wa Denmark kwa lengo la kupambana na umaskini na kukuza haki za binadamu. Ukuaji wa uchumi ni dhana muhimu ya mkakati huu lakini ukuaji huo unapaswa kuzingatia udhibiti wa mazingira na kukuza maendeleo ya kijamii ili yachangie katika kuboresha maisha ya watu  maskini na kujenga uwezo wao. Watu wote wana haki ya kuishi na kuwa na fursa sawa. Haki za binadamu kwa hiyo  ni uti wa mgongo wa mkakati huu. Mradi utasimamia utekelezaji wa hatua madhubuti za maendeleo na ustawi wa jamii.

Mkakati huu unalenga katika kumiliki matokeo na kuwepo kwa uwazi wa usimamizi wa ushirikiano wa kimaendeleo. Ushirikiano wa kimaendeleo wa Denmark ni lazima  uendane na mazingira ya nchi  ambazo zinapewa kipaumbele wadau wa kimataifa, sekta binafisi na asasi za  kijamii. Denmark  ina lengo la kuwa na ushirikiano na mataifa mbalimbali  katika sera yake ya  maendeleo. Hata hivyo juhudi hizi zitaelekezwa zaidi katika nchi maskini ambapo  mahitaji ni makubwa na ambako Denmark inaweza kuleta mbadiliko.


Biashara, Afya, Usafiri, Utawala Bora – Haya ni maeneo ya kipaumbele katika ushirikiano na Tanzania. Kushoto kuna orodha yenye taarifa ya ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.

Mkakati wa Msaada wa Maendeleo Tanzania

Kwa miaka kadhaa, Tanzania imekuwa moja ya nchi zinazoongoza katika kupokea misaada ya maendeleo kutoka Denmark. Denmark ni miongoni mwa wahisani wakubwa wa maendeleo nchini Tanzania.

Kazi kubwa nchini ni kuchangia katika maeneo yafuatayo: 

  1. Kukuza uchumi ulio endelevu na wenye uwiano katika jamii;
  2. Kuboresha hali ya maisha ya watu maskini;
  3. Kukuza utekelezaji wa kuboresha mazingira, ajira na;
  4. Kuimarisha maadili ya kidemokrasia, utawala bora, utawala wa sheria, na kuheshimu haki za binadamu.

Upande wa kushoto utapata taarifa zifuatazo:  

  • Taarifa zaidi kuhusu mipango mbalimbali;
  • Kwa nini ubalozi wa Denmark unajikita zaidi katika sekta zilizotajwa hapo juu na nini ni mafanikio ya kazi hizo;
  • Nyaraka  kuhusu mpango na nyaraka za ziada kwa taarifa zaidi  bofya tovuti husika;
  • Taarifa za watumishi wa Ubalozi wanaohusika na mpango wa maendeleo.

Unaweza pia kusoma kuhusu ubia wa kibiashara ya Tanzania na Denamrk pamoja na miradi ya utafiti nchini Tanzania inayofadhiliwa na DANIDA.

Mwisho, unaweza kupata taarifa kuhusu vipaumbele vya kisiasa na sera maendeleo za DANIDA na mkakati wa pamoja kwa ajili ya ushirikiano wa maendeleo iliyoandaliwa na Serikali ya Tanzania na Washirika wa Maendeleo.